Swahili - Surah Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) | المكتبة الإسلامية صدقة جارية عن المغفور لهم بإذن الله أحمد سليمان البراك وزوجته وابنائه سليمان ومحمد ويونس وابنته إيمان

,,

اللهم اجعل هذا العمل نافعاً لصاحبه يوم القيامة

ولمن ساهم وساعد بنشره

,,

Surah Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder)

Swahili

Surah Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya count 25
Facebook Twitter Google+ Pinterest Reddit StumbleUpon Linkedin Tumblr Google Bookmarks Email
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ( 1 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 1
Itapo chanika mbingu,
وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ( 2 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 2
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ ( 3 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 3
Na ardhi itakapo tanuliwa,
وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ ( 4 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 4
Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu,
وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ( 5 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 5
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ ( 6 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 6
Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.
فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ ( 7 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 7
Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,
فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ( 8 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 8
Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi,
وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا ( 9 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 9
Na arudi kwa ahali zake na furaha.
وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ ( 10 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 10
Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,
فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا ( 11 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 11
Basi huyo ataomba kuteketea.
وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا ( 12 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 12
Na ataingia Motoni.
إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا ( 13 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 13
Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.
إِنَّهُ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ ( 14 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 14
Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.
بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا ( 15 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 15
Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ ( 16 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 16
Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ ( 17 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 17
Na kwa usiku na unavyo vikusanya,
وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ ( 18 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 18
Na kwa mwezi unapo pevuka,
لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ ( 19 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 19
Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!
فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ( 20 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 20
Basi wana nini hawaamini?
وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ۩ ( 21 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 21
Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu?
بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ ( 22 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 22
Bali walio kufuru wanakanusha tu.
وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ ( 23 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 23
Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.
فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ( 24 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 24
Basi wabashirie adhabu chungu!
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ( 25 ) Al-Inshiqaq (The Splitting Asunder) - Aya 25
Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.
Facebook Twitter Google+ Pinterest Reddit StumbleUpon Linkedin Tumblr Google Bookmarks Email

Select language

Select surah