Swahili - Surah Abasa ( He frowned ) | المكتبة الإسلامية صدقة جارية عن المغفور لهم بإذن الله أحمد سليمان البراك وزوجته وابنائه سليمان ومحمد ويونس وابنته إيمان

,,

اللهم اجعل هذا العمل نافعاً لصاحبه يوم القيامة

ولمن ساهم وساعد بنشره

,,

Surah Abasa ( He frowned )

Swahili

Surah Abasa ( He frowned ) - Aya count 42
Facebook Twitter Google+ Pinterest Reddit StumbleUpon Linkedin Tumblr Google Bookmarks Email
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ( 1 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 1
Alikunja kipaji na akageuka,
أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ ( 2 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 2
Kwa sababu alimjia kipofu!
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ ( 3 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 3
Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ ( 4 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 4
Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ ( 5 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 5
Ama ajionaye hana haja,
فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ ( 6 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 6
Wewe ndio unamshughulikia?
وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ( 7 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 7
Na si juu yako kama hakutakasika.
وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ ( 8 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 8
Ama anaye kujia kwa juhudi,
وَهُوَ يَخْشَىٰ ( 9 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 9
Naye anaogopa,
فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ ( 10 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 10
Ndio wewe unampuuza?
كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ ( 11 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 11
Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ( 12 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 12
Basi anaye penda akumbuke.
فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ( 13 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 13
Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ ( 14 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 14
Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
بِأَيْدِي سَفَرَةٍ ( 15 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 15
Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
كِرَامٍ بَرَرَةٍ ( 16 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 16
Watukufu, wema.
قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ ( 17 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 17
Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ( 18 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 18
Kwa kitu gani amemuumba?
مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ ( 19 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 19
Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ ( 20 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 20
Kisha akamsahilishia njia.
ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ ( 21 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 21
Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ ( 22 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 22
Kisha apendapo atamfufua.
كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ ( 23 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 23
La! Hajamaliza aliyo muamuru.
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ ( 24 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 24
Hebu mtu na atazame chakula chake.
أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا ( 25 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 25
Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا ( 26 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 26
Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا ( 27 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 27
Kisha tukaotesha humo nafaka,
وَعِنَبًا وَقَضْبًا ( 28 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 28
Na zabibu, na mimea ya majani,
وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا ( 29 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 29
Na mizaituni, na mitende,
وَحَدَائِقَ غُلْبًا ( 30 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 30
Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
وَفَاكِهَةً وَأَبًّا ( 31 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 31
Na matunda, na malisho ya wanyama;
مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ( 32 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 32
Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ ( 33 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 33
Basi utakapo kuja ukelele,
يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ( 34 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 34
Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ( 35 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 35
Na mamaye na babaye,
وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ( 36 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 36
Na mkewe na wanawe -
لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ( 37 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 37
Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ ( 38 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 38
Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ ( 39 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 39
Zitacheka, zitachangamka;
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ ( 40 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 40
Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ ( 41 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 41
Giza totoro litazifunika,
أُولَٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ ( 42 ) Abasa ( He frowned ) - Aya 42
Hao ndio makafiri watenda maovu.
Facebook Twitter Google+ Pinterest Reddit StumbleUpon Linkedin Tumblr Google Bookmarks Email

Select language

Select surah