Swahili - Surah At-Takwir ( The Overthrowing ) | المكتبة الإسلامية صدقة جارية عن المغفور لهم بإذن الله أحمد سليمان البراك وزوجته وابنائه سليمان ومحمد ويونس وابنته إيمان

,,

اللهم اجعل هذا العمل نافعاً لصاحبه يوم القيامة

ولمن ساهم وساعد بنشره

,,

Surah At-Takwir ( The Overthrowing )

Swahili

Surah At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya count 29
Facebook Twitter Google+ Pinterest Reddit StumbleUpon Linkedin Tumblr Google Bookmarks Email
إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ( 1 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 1
Jua litakapo kunjwa,
وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ ( 2 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 2
Na nyota zikazimwa,
وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ ( 3 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 3
Na milima ikaondolewa,
وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ ( 4 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 4
Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe,
وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ ( 5 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 5
Na wanyama wa mwituni wakakusanywa,
وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ ( 6 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 6
Na bahari zikawaka moto,
وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ ( 7 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 7
Na nafsi zikaunganishwa,
وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ ( 8 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 8
Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa,
بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ ( 9 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 9
Kwa kosa gani aliuliwa?
وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ ( 10 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 10
Na madaftari yatakapo enezwa,
وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ ( 11 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 11
Na mbingu itapo tanduliwa,
وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ ( 12 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 12
Na Jahannamu itapo chochewa,
وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ ( 13 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 13
Na Pepo ikasogezwa,
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ ( 14 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 14
Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha.
فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ ( 15 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 15
Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma,
الْجَوَارِ الْكُنَّسِ ( 16 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 16
Zinazo kwenda, kisha zikajificha,
وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ ( 17 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 17
Na kwa usiku unapo pungua,
وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ ( 18 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 18
Na kwa asubuhi inapo pambazuka,
إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ( 19 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 19
Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu,
ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ( 20 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 20
Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi,
مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ( 21 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 21
Anaye t'iiwa, tena muaminifu.
وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ ( 22 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 22
Na wala huyu mwenzenu hana wazimu.
وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ ( 23 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 23
Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.
وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ ( 24 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 24
Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu.
وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ ( 25 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 25
Wala hii si kauli ya Shetani maluuni.
فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ ( 26 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 26
Basi mnakwenda wapi?
إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ( 27 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 27
Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ ( 28 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 28
Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa.
وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ( 29 ) At-Takwir ( The Overthrowing ) - Aya 29
Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Facebook Twitter Google+ Pinterest Reddit StumbleUpon Linkedin Tumblr Google Bookmarks Email

Select language

Select surah